Dibaji

Jamii ya binadamu ni mkusanyiko wa familia nyingi. Uislamu unatilia maanani sana kwenye furaha halisi na ufanisi wa wanadamu kwa njia ya ulinganifu wa Kiislamu, maadili ya hali ya juu, familia zenye elimu, na zenye tabia nzuri na nyumba zenye furaha. Kama ilivyo katika maeneo yote ya shughuli za binadamu, Uislamu umeweka wazi na kinaganaga haki na wajibu wa wanaume na wanawake, waume na wake (walio kwenye ndoa) na pia wazazi na watoto.

Familia zenye furaha zilizo na mazingira yenye kufurahisha, ambamo mume, mke na watoto na ndugu wengine huishi pamoja kwa uchangamfu na uelewano wa pande mbili, ustahamilivu na heshima na kutimiza wajibu wao kwa ihusikavyo kwa kila mmoja wao, kwa hakika ni kielelezo cha hadhi ya juu zaidi ambacho Mweyezi Mungu Mweza wa yote amewabariki wanadamu miongoni mwa viumbe wote.

Kwa bahati mbaya, upungufu wa kutokufahamu vipengele hivi, hususan kwa waume na wanawake, husababishia kwenye matatizo mengi kwao wenyewe na halikadhalika kwa watoto - vizazi vijavyo. Kwenye nchi za magharibi zilizoendelea, zenye kupiga hatua zaidi, mafanikio makubwa zaidi ya kiteknolojia, kisayansi na mwenendo wa maisha ya kasi ya kisasa zaidi; huko kiwango cha kutalikiana na kutengena kinatisha.

Kwa kulichukulia umuhimu wa somo hili, ICRO (Kitengo cha utamaduni cha Kiislamu - Iran) kinachukuwa fursa ya kuchapisha kitabu hiki (kwa asilia katika lugha ya Kifursi) kilichoandikwa na msomi maarufu wa Kiislamu, mwandishi mwenye kujulikana Profesa mwandamizi wa maarifa ya sheria za Kiislamu katika Hawzah Ilmiyah (Islamic Theological Centre), Qum, Iran, Hujjatul-Islam

Ibrahim Amini. Mwandishi amefanya jitihada kubwa katika kufanya utafiti na uchunguzi wa kina wa somo la mfumo wa maadili ya familia na uhusiano wa mume na mke.

Sehemu ya kwanza inaongelea wajibu wa wanawake na sehemu ya pili inaongelea wajibu wa wanaume.

Pamoja na wajibu, haki za waume kwa wake na zile za wake kwa waume pia zimeelezewa kwa kunukulu Aya za Quran Tukufu na Hadith.

Ni matumanini yetu kwamba kitabu kitakuwa chenye manufaa kwa wote na kila familia itakifanya kuwa hazina ya kupata faida ya upeo wa juu sana katika kuanzisha na kudumisha mazingira safi na ya kufurahisha, yaliyojaa baraka za Mwenyezi Mungu.

Department of Translation and Publication,
Islamic Culture and Relations Organization